Rais Dkt.Samia afanya uteuzi wa Balozi,Posta Masta Mkuu, avunja bodi

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

ii) Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

iii) Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 25, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ambapo uteuzi huu unaanza mara moja na Balozi Mteule Bw. Ulanga ataapishwa tarehe 26 Septemba, 2023 Ikulu, Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news