Sanjay Dutt atua nchini kufanya Royal Tour

NA JOHN MAPLEPELE

MSANII maarufu duniani kwenye eneo la filamu kutoka nchini ambaye ana zaidi ya wafuasi milioni mia mbili katika mitandao yake, Sanjay Dutt leo Septemba 18, 2023 ametua kuanza Royal Tour hapa nchini.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokewa na Mkurugenzi wa Utalii nchini Dkt.Thereza Mugobi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Damasi Mfugale,Dutt amesema, ameamua kuja kutembelea vivutio vya utalii nchini kufuatia Filamu ya The Royal Tour iliyochezwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuonyesha hazina ya utajiri wa vivutio vya utalii nchini.

"Naipenda sana Tanzania, naiona niifanye Tanzania kuwa nyumba yangu ya pili sasa baada ya kuitazama filamu ya The Royal Tour," amesisitiza Dutt.

Aidha, amesema ameamua kuwa balozi wa kujitolea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mitandao yake kutokana na mapenzi yake kwa Taifa la Tanzania.

Mkurugenzi wa Utalii nchini, Dkt.Thereza Mugobi amefafanua kuwa Tanzania imefarijika kupata ugeni wa msanii huyo maarufu duniani kutoka India eneo ambalo lina idadi kubwa ya watu takribani bilioni 1.4 ambao ni soko la kimkakati la Tanzania.

"Ujio wa Dutt ni faraja kwetu kwa vile tunatambua itasaidia kuwa vuta wageni wengi kutoka bara la Asia ambako yeye anawafuasi wengi,"ameongeza Dkt.Mugobi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Damasi Mfugale amesema Serikali itaendelea kuwakaribisha watu maarufu duniani ili wasaidie kufikia azma ya kufikisha wageni milioni tano ifikapo 2025 na kuliingizia Taifa dola bilioni Sita za kimarekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news