Serikali yatoa maelekezo wanaokaimishwa nafasi

NA LUSUNGU HELELA

WATENDAJI katika Taasisi za Umma wamesisitizwa kuwakaimisha nafasi za madaraka watumishi wenye sifa za kushika nafasi hizo ili kuirahisishia kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI kutekeleza hatua zinazofuata kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akizungumza na Watumishi wa Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara, ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kuzungumza na kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao.

Hayo, yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Mara katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa umma. 
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Said Mtanda akizungumza na Watumishi mara baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete kuzungumza nao ambapo amewataka Watumishi hao kufanya kazi kwa bidii.

"Tunawavunja moyo watumishi wenye sifa kwa kuwa baadhi ya viongozi wanakaimisha ofisi kwa watumishi wanaowataka wenyewe na kwa mapenzi binafsi na kusahau kuwa nafasi hizo zipo kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia sifa na vigezo,’’amesema Mhe. Kikwete. 

Katika hatua nyingine, Mhe. Kikwete amewataka Maafisa Utumishi kufanya kazi zao kwa weledi na kuhakikisha wanafuatilia masuala ya watumishi wao ikiwa ni pamoja maslahi, upandishwaji vyeo na stahiki mbalimbali. Mhe. Kikwete yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani humo na kusikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili ili kuzitatua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news