Simba SC waitumia Coastal Union kujiandaa na Power Dynamos

DAR ES SALAAM-Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema, wameutumia mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union kujiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Robertinho amesema, katika mchezo wa leo ambao umepigwa katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam amewatumia wachezaji wenye uzoefu ili kuzidi kutengeneza maelewano baina yao kuelekea mechi dhidi ya Power Dynamos itakayopigwa Oktoba Mosi, mwaka huu.

Pia ameweka wazi kuwa amefurahishwa na jinsi wachezaji walivyocheza ingawa anaamini walikuwa na nafasi ya kupata mabao mengi zaidi ya matatu waliyofunga.

“Tumeutumia mchezo wa leo kujiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos. Tulijua Coastal watatupa mechi ngumu ambayo itazidi kutuimarisha.

“Ukiangalia kikosi cha leo tumewatumia wachezaji wenye uzoefu ambao tunategemea kuwatumia dhidi ya Power Dynamos,”amesema Robertinho.

Akizungumzia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal, Robertinho amesema, “tulikuwa na nafasi kubwa ya kupata mabao sita mpaka saba, lakini matatu sio mbaya, nawapongeza wachezaji wangu.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news