Simba SC yatembeza kichapo kwa Pan African

DAR ES SALAAM-Kikosi cha Simba SC kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pan African katika mchezo wa kirafiki.

Ni kupitia mtanage wa nguvu ambao ulipigwa Septemba 26, 2023 katika Uwanja wa Mo Simba Arena jijini Dar es Salaam ambao umechezwa katika vipindi vitatu yaani dakika 30 kila kipindi.

Said Ntibazonkiza aliwapatia waajiri wake bao la kwanza dakika ya 35 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Aidha, Moses Phiri awapatia waajiri wake bao la pili dakika ya 65 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo mshambuliaji, Willy Essomba Onana.

Vile vile, Kibu Denis aliwapatia waajiri wake bao la tatu dakika ya 70 kufuatia Onana kuukosa mpira akiwa ndani ya 18 kabla ya kumkuta.

Hata hivyo, Onana alikamilisha ratiba kwa kufunga bao la nne dakika ya 87 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Phiri, hivyo hadi mwisho wa mchezo, wenyeji waliichakaza Pan African mabao 4-0.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news