TBA yathamini mchango wa watendaji wakuu wastaafu

DAR ES SALAAM-Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umefanya tafrija fupi na kuwakabidhi tuzo ya pongezi watendaji wakuu wastaafu kama sehemu ya kutambua mchango wako wakati wa utumishi wao.

Akizungumza wakati wa tafrija hiyo, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amewashukuru watendaji wakuu hao wastafu kwa kukubali kujumuika pamoja na wana TBA waliopo kazini.

Pia, Arch. Kondoro amewashukuru kwa kuweka misingi mizuri inayowawezesha waliopo kazini kuendeleza yale yote yaliyoachwa na watangulizi wake.

Aidha, Arch. Kondoro amewaeleza jitihadi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zinazopelekea kutekelezwa kwa miradi mingi zaidi ikiwa ni pamoja na mradi ya ujenzi wa nyumba 3500 katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma ambapo kwa heshima mitaa imepewa majina yao.

Akizungumza katika tafrija hiyo, Arch. Makumba Togalai Kimweri aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa TBA kati ya mwaka 2002 mpaka 2011 amesema, “Nashukuru kwa kutukumbuka.

"Nilikaribishwa Arusha kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Makazi la Kibiashara. Nilifurahi kuona miradi niliyoiacha inakamilishwa. Tumuunge sana mkono Mtendaji Mkuu kwenye nafasi yake. Niwatakie heri sana kwa kazi mnaiyoifanya.”

Naye Eng. John Ainainyi Njau aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa TBA kati ya mwaka 2011 na 2012 amesema, “Mnafanya vizuri zaidi ya tulivyofanya kuendeleza taifa letu. Tunajivunia sana kwa mnachoendelea kufanya.”

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanya tafrija na kutoa Tuzo ya Pongezi kama ishara ya kuenzi mchango na msingi mzuri ulioachwa na viongozi hao wastaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news