Mwinjilisti Temba ampa kongole Rais Dkt.Samia, amtaja Biteko

DAR ES SALAAM-Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akiendelea kuimarisha safu ya uongozi serikalini ili iweze kuwafikia wananchi na kuwahudumia, Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amempongeza kwa juhudi hizo.

Temba ambaye ni kati ya Watanzania wachache wenye wito wa kipekee katika kulihubiri na kueneza neno la Mungu ndani na nje ya nchi, pia ni kati ya watumishi wa Mungu ambao wamepewa kibali cha namna yake cha kuhimiza mshikamano, upendo, amani na umoja kwa jamii.

Akizungumza leo Septemba 3, 2023 jijini Dar es Salaam,Mwinjilisti Temba amesema kuwa, Rais Dkt.Samia amekuwa na maono makubwa ya kuwapa nafasi Watanzania wachapa kazi nafasi ili waweze kumsaidia kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

"Mimi, ndugu Alphonce Temba ambaye ni Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupanga safu ya viongozi.

"Viongozi ambao ni wachapa kazi,na kuendelea kuboresha maslahi ya Taifa kwa kuzingatia kwamba wananchi mbalimbali wenye changamoto, changamoto zao mbalimbali zinaendelea kutatuliwa kwa wakati kupitia viongozi wachapa kazi ambao amekuwa akiwaamini na kuwapa majukumu katika nafasi mbalimbali.

"Ni katika mabadiliko aliyoyafanya hivi karibuni, hata hivyo nimpongeze zaidi kwa kumchagua Dkt.Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati."

Biteko ni nani?

"Na leo hii ninataka kumuelezea Biteko. Dkt.Biteko ni mtumishi ambaye ana roho ya unyenyekevu,ana utii kwa kila mtu pasipokuwangalia umri au cheo, ni mfano wa kuigwa wa mawaziri,katika karne hii yetu.
 
 
Mwinjilisti Temba pia ameelezea tofauti kubwa ya Naibu Waziri Mkuu Dkt.Buteko na baadhi ya watumishi wengi kuwa ni tabia yake ya kuisikiliza watu pande zote bila kuhukumu kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wengi kuwa na viburi na kutokusikiliza watu jambo ambalo linazidi kumjengea heshima ya kipekee.

"Na katika Taifa letu la Tanzania ni kati ya viongozi walioshika nafasi kubwa wakiwa wadogo, lakini kwa nidhamu kubwa, kwa maskini na matajiri kwa hekima kubwa, bila ubaguzi.

"Amekuwa na maneno ya hekima kubwa kinywani mwake katika kunena, amekuwa akinena kwa tafakari kubwa, mwaka 2019 alinialika katika ofisi yake Dodoma.

"Ambapo pamoja na mamboo mengine nilikwenda kumshauri juu ya biashara ya madini, hasa katika madini ya vito ambako kulikuwa hakuna,bei elekezi, hata hivyo (Dkt.Biteko) alinikutanisha na Mwenyekiti wa Bodi, nilivyokaa naye ikagundulika kabisa kwamba Serikali ilikuwa haijaandaa bei elezi ya game stones.
 
"Kwa hiyo nikamshauri Mwenyekiti kuwa, ni vizuri wakawaona wafanyabiashara wazoefu wakapata majina na gharama za kila jiwe ili Serikali iweze kupanga bei ya game stones.

"Ilikuwa ni kabla ya kwenda kumshauri Rais Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu ulikuwa ni mkutano kati ya viongozi wa dini juu ya uanzishwaji wa masoko ya madini ambayo aliyafanya muda mfupi baada ya mkutano wetu wa viongozi wa dini na Rais Dkt.Magufuli."

"Mkutano huo ulifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, na katika kikao kile nilipata nafasi ya kumuuliza maswali na kumuomba amkaribishe mwekezaji kutoka Thailand ambaye alitaka kuja kufungua biashara kadha w kadha, kuleta wafanyabiashara.

"Kuleta minada ya madini nchini ambapo Mheshimiwa Magufuli alikubaliana na hoja zangu na akatoa maelekezo kwamba mtu huyu aletwe haraka Ikulu na ikiwezekana amuone Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au yeye (Magufuli) ili aweze kuleta soko la madini nchini na wawekezaji mbalimbali.

"Hata hivyo, niligonga mwamba,baada ya kupewa maelekezo ya barua kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi kufuata utaratibu mpya ambao, nilipofuatilia utaratibu ulishindikana kabisa kumleta mwekezaji yule ambaye alikuwa tayari, mpaka sasa hivi anatamani kuja kufungua biashara kubwa nchini na wafanyabiashara.

"Kwa sababu pamoja na mambo mengine kulikuwa kunaombwa kuwepo ubalozi kati ya Thailand na Tanzania ambao Wathailand walikuwa wamemuomba Rais Magufuli (hayati) kufunguliwa kwa ubalozi ili kuwa rahisi kwao kuja kufanya biashara hapa nchini, kwa sababu.

"Wao wakitaka kuja Tanzania ama waende India ama kupitia Nairobi nchini Kenya na ndiyo maana soko la Tanzanite linaonekana linatokea Kenya kwenda Thailand kwa sababu lazima ndege, lazima ipitie Nairobi nchini Kenya.

"Na ndiyo maana wanaona kwamba, Tanzanite inatoka Nairobi na si Wakenya kujifanyisha, kwa sababu hatuna ubalozi wa moja kwa moja na vitu vinavyoandikishwa vyote kutoka Airports zao zinaonekana kutoka Nairobi kutoka Afrika Mashariki.

"Afrika na kutoka Tanzania, baada ya yale mazungumzo yangu pamoja na Mwenyekiti wa Bodi halafu baadae nikarudi ofisini kwa waziri,waziri aliniahidi kuyafanyia kazi, mambo hayo japo sijajua mpaka sasa hivi kama bado wizara ina wasiwasi kama Wizara ya Madini ina bei elekezi ya madini ya vito.

Miongoni mwa madini ya vito ambayo yanapatikana hapa nchini ni sapphire, ruby, emerald, spinel, tanzanite, alexandrite, tourmaline, zircon, aquamarine, tsavorite, spessartite, rhodolite na mengineyo.

"Baada ya kurudi Dar es es Salaam na baada ya muda kidogo, Mungu alinipa ujumbe kupitia kwa Waziri Biteko (Waziri wa Madini) juu ya maisha yake, kazi yake na nini Mungu anataka afanye, na hata mitego ambayo ilikuwa mbele yake ambayo nilipaswa kuivunja na kuomba juu yake.

"Nilimshirikisha na nilimfanyia maombi maalumu, na alituma sadaka na kwa kuwa maadiko yanasema wazi katika kitabu cha 2Mambo ya Nyakati 20:20, kwamba muwaamini watumishi ili muweze kufanikiwa, na mumwaamini Mungu akuthibitishe, kwa hiyo alituma sadaka yake na kupitia sadaka yake.

"Nilimfanyia maombi maalumu sana na nikafungua kabisa malango yake, na haya anayoyapata sasa ni matokeo ya sadaka aliyonipa, kama vile sadaka aliyoitoa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2004 kama vile sadaka aliyoitoa Michael Satta mwaka 2007.

"Kama vile sadaka walizozitoa watu wengi na sadaka aliyoitoa Raila Odinga mwaka 2022, kwa hiyo nataka nitoe wito hasa kwa wanaopewa madaraka, viongozi wakubwa hasa mawaziri wasipandishe mabega juu kwa nafasi wanazozipata wakawa na wananchi, wakajisahau wakaona kama walistahili hawatafika mbali.

"Wapo watu wengi ambao ninawaheshimu na niliwatabiria wakapata nafasi, Mbunge wa Chalinze, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete mwaka mmoja kabla nilimtabiria kuwa Mbunge na akawa Mbunge.

"Wako watu wengi sana, sisemi hadharani mambo yao, lakini wapo watu wengi sana wanaokutana na mimi ninavyowaombea mfano Freeman Mbowe alipokamatwa wiki ya kwanza nilikwenda Magereza.

"Wiki ya kwanza alipokamatwa akiwa Magereza, nilimwambia ataachiwa huru, soon na akaachiwa nilipewa melekezo na Roho Mtakatifu, nikafanya hiyo kazi ikatokea.

"Nimesema kabisa wazi, Katiba mpya itakuwa baada ya uchaguzi 2025 na itakuwa, ingekuwa tayari imeshapatikana, lakini hayo mengine yamejiibua, mambo ya bandari, mambo ya nini yamejiibua, yanazuia Katiba mpya isipatikane sasa,

"Ili ifike wakati mtumishi wa Mungu aheshimike tena, kama siyo suala la bandari ingekuwa sasa hivi tupo kwenye mchakato wa katiba, mchakato wa katiba mpya hatuwezi kwenda bila kupatikana fedha,na fedha itatoka Bunge la kesho na Bunge la kesho litaandaa mchakato wa uchaguzi wa mwaka kesho kutwa.

"Kwa hiyo Katiba mpya haitakuwa kabla ya 2025 ni baada ya 2025 ndiyo itatokea na haya yote niliyanena,na hii ipo kwenye page kwenye U-Tube na Mungu hajawahi kuliangusha neno langu,na halitaanguka. Amen,"amefafanua kwa kina Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news