Vyandarua vinavyosambazwa na MSD viko salama- DC wa Nzega

TABORA-Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitwapwaki Tukai amesema ,hatakubali kuona jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuboresha maisha ya Watanzania na sekta ya afya zinarudishwa nyuma kwa makusudi, hususani kwa kukwamisha mradi wa usambazaji wa vyandarua kwa wananchi.

Ameongeza iwapo atabaini mtu anauza au kufugia kuku vyandarua kwa kisingizio kuwa vinapunguza nguvu za kiume hatamvumilia, na mwananchi atakayehujumu atalazimika kutoa vyandarua vingine 10.

“Niwatake wanawake wenzangu msikubali kudanganywa na kukimbiwa kitandani, mwanaume hawezi kukosa nguvu kwa kulala katika neti yenye dawa kama huna nguvu huna tu,”alisisitiza.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kulinda familia zao kwa kuwa hakuna kiongozi wa nchi anayetaka kuona anapoteza nguvu kazi yake hivyo, Rais Dkt.Samia anajua thamani ya Watanzania.

Naye Richard Sendela mkazi wa Utemi Nzega Mjini, ameeleza kuwa vyandarua hivyo ni muhimu hivyo, wanaishukuru serikali kwa kuwafikia wale wenye hali ya chini ambao hawakuwa na uwezo wa kununua vyandarua vya familia nzima kwa kaya.

Naye Kaimu Meneja wa MSD Tabora, Adonizedeck Tefurukwa, aliwahakikishia wananchi wa Nzega kuwa wote walio katika mpango wa kupewa vyandarua hivyo baada ya kujiandikisha katika kaya zao watapata, kwani vipo vya kutosha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news