Wajadili namna ya kuboresha mifumo ya chakula Afrika

DAR ES SALAAM-Wabunge 19 kutoka nchi nane za Afrika wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili namna bora ya kuboresha mifumo ya kilimo, na usalama wa chakula kwenye nchi za Afrika ikiwa ni jitihada za kuondokana na utegemezi wa chakula kutoka nchi za nje.
Akizungumza kwa niaba ya Bunge la Tanzania, Mariam Mzuzuri ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki Elimu, Mifugo, Viwanda na Biashara amesema , ni jambo jema kwa nchi za Afrika kuungana ili kuwekeza nguvu ya pamoja kwenye kuboresha mifumo ya chakula Afrika.

Mzuzuri amesema, Bara la Afrika lina ardhi kubwa ambayo inaweza kutumika kwa kila aina ya uzalishaji wa chakula na kuondokana na uagizaji wa chakula kutoka nje ya nchi

Ameongeza kuwa, Tanzania imekuwa ikichukua hatua kila siku ili kuinua mifumo ya kilimo nchini mabapo katika miaka miwili iliyopita ya bajeti kumekua na ongezeko la asilimia zaidi ya 100 ili kukidhi mahitaji ya sekta hiyo muhimu zaidi nchini.

Mkutano huo pia umelenga kuongeza muunganiko wa sera na fursa za pamoja kwa nchi za Afrika ili kuweza kuanzisha mfumo utakaotumika kukabiliana na changamoto zinazolikumba Bara la Afrika kiasi cha kushindwa kuzalisha chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya watu wake

"Nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikikumbana na changamoto ya ukosefu wa chakula kwa sababu ya kukosa mifumo sahihi ya usalama wa chakula, hivyo muungano wa wabunge hawa watakwenda kuishauri serikali yale ambayo tumeafikia ili kuleta mabadiliko chanya katika mifumo yetu,"amesema Mzuzuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news