Bei ya Diezeli yapaa Zanzibar

ZANZIBAR-Mamlaka ya Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ( ZURA) imetangaza bei mpya ya mafuta huku Dizeli ikipaa kwa asilimia tisa kutokea mwezi Septemba hadi Oktoba, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano cha mamlaka hiyo imesema, bei ya Petroli kwa Oktoba lita 1 itauzwa shilingi 3,001 ambapo Septemba ilikuwa ni shilingi 2,950 ikiwa ni tofauti ya shilingi 51.

Aidha,Dizeli mwezi Septemba ilikuwa lita moja ni shilingi 3,012 ambapo kwa mwezi huu wa Oktoba ni shilingi 3,282 hii ikiwa ni ongezeko la shilingi 270 sawa na asilimia tisa.

Wakati huo huo, mafuta ya taa kwa mwezi Septemba na Oktoba imeendelea kusalia katika bei Ile Ile ya shilingi 2,921 kwa lita moja.

Vile vile, mafuta ya ndege kwa mwezi wa Septemba lita ilikuwa ni shilingi 2,448, imepanda kwa shililingi 320, hivyo kwa mwezi huu wa Oktoba yanauzwa kwa shilingi 2768 kwa lita moja.

ZURA imesema kupanda huko kunatokana na kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la Dunia, gharama za uingizaji wa mafuta, uamuzi wa wazalishaji wa Mafuta Duniani (OPEC) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo Taifa la Urusi imewekewa na mataifa ya Magharibi.Bei hizo mpya za mafuta zimeanza kutumika kuanzia Oktoba 8, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news