HII HAPA ORODHA YA WATUMISHI 5,740 WALIOPATA VIBALI VYA UHAMISHO KWA MAOMBI YA KUANZIA MWEZI JANUARI HADI JULAI, 2023

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Adolf H. Ndunguru ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa watumishi 5,740 walioomba kuhamia kwenye halmashauri mbalimbali nchini.

Bw. Ndunguru amesema Ofisi yake imefanyia kazi maombi yote ya uhamisho yaliyowasilishwa kuanzia mwezi Januari hadi Julai, 2023.

Aidha amewataka watumishi waliokuwa katika orodha ya uhamisho katika tangazo lililotolewa Januari 21, 2023 na hadi sasa hawajapata vibali vya uhamisho wafike kwenye ofisi za halmashauri zao kwa kuwa vibali hivyo vimeshatumwa.

Pia amewataka watumishi wote waliopata uhamisho wa kubadilishana kuwa hawaruhusiwi kuomba kufuta uhamisho baada ya barua za uhamisho kutoka kwani tayari mtumishi anayebadilishana naye amesharipoti katika kituo kipya cha kazi.

Halikadhalika amesisitiza kuwa watumishi wote waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye halmashauri zao na sio kwenda Ofisi ya Rais–TAMISEMI kufuata barua hizo.

Pia amewataka Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa vibali vya uhamisho kwa watumishi hao waliokamilisha mchakato na kupata vibali vya uhamisho kwani uhamisho ni haki ya kila mtumishi.

Mwisho amewataka watumishi wote wanaoomba uhamisho kuzingatia taratibu zote za uhamisho kama ilivyoainishwa kwenye Waraka wa Watumishi Na. 2 wa mwaka 2018 na maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais–Utumishi aliyoyatoa kupitia barua yenye Kumb Na. FA.228/613/01/1 ya tarehe 11 Agosti, 2023.Hapa chini ni orodha ya watumishi waliopata vibali vya uhamisho kama ifuatavyo;


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news