Rais Dkt.Samia ataka nidhamu kwa watumishi wa umma

MANYARA-Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa Umma kuwa na nidhamu katika utendaji kazi wao kwa Wananchi ili kuondokana na Malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara katika taasisi mbalimbali.

Rais, Samia ameyasema hayo Oktoba 14 katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 zilizofanyikia katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo katika mji wa Babati mkoani Manyara.

“Kumekuwa na malalamiko ya Wananchi kuhusu matumizi ya lugha chafu, kucheleweshwa kwa huduma au kudaiwa rushwa na hili ninawataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya mlibebe ipasavyo maana huko chini ndio kwenye shida kubwa,”amesema Rais Dkt.Samia.

Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa ya kilimo biashara, kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza tatizo la ajira nchini

Kwa upande wake Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango amesema kuwa, jitihada za makusudi za utunzaji wa mazingira zinahitajika ili kulinda na kutunza mazingira kwa vizazi vijavyo.

Akiwakilisha salamu za Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema zaidi ya Sh bilioni 535.7 zimetolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya maji,barabara Elimu pamoja Afya.

Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2024 utazinduliwa mkoani Kilimanjaro na kilele cha mbio hizo pamoja na wiki ya vijana itafanyika mkoani Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news