Hizi hapa nafasi za ajira kutoka Jeshi la Polisi Tanzania

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Kujenga Uchumi (JKU), waliopo kwenye makambi na nje ya makambi wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Kidato cha nne.

1. Sifa za Waombaji
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b) Awe amehitimu kidato cha nne au cha sita kuanzia mwaka 2017 hadi 2022.
c) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
d) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 29.
e) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe wamesoma masomo ya sayansi na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka la tatu (Division I – III)
f) Wahitimu wa Shahada, Stashahada na Astashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 29.
g) Awe na urefu usiopunguwa futi tano na inchi tano (5’5”) kwa wanaume, na futi tano inchi mbili (5’2”) kwa wanawake.
h) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
i) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
j) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
k) Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.
l) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
m) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
n) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
o) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
p) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
q) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
r) Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8), Stashahada (NTA level 6) na Astashadaha (NTA Level 5 au NVA Level 3) wanatakiwa wawe na fani
zilizoainishwa kwenye tangazo.

2. Utaratibu wa kutuma Maombi

1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono
(Handwriting) bila kusahau namba za simu, na watumie anuani ya Mkuu wa Jeshi la
Polisi S.L.P 961 DODOMA.
2. Waombaji wote waambatanishe nakala zifuatazo:
a) Nakala ya cheti cha kuzaliwa
b) Nakala ya kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA
c) Nakala ya cheti cha kuhitimu mafunzo ya JKT/JKU kwa walio nje ya makambi.
d) Nakala za vyeti vya taaluma (Academic Certificates).
e) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya sekondari (Leaving Certificate).

3. Kwa waombaji wa kidato cha sita na cha nne ambao wamehitimu mafunzo ya JKT/JKU waliopo nje ya makambi (uraiani) maombi yao yapelekwe kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliopo na sio Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

4. Kwa waombaji wa kidato cha sita na cha nne waliopo kwenye makambi ya JKT/JKU
maombi yao yawasilishwe kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kupitia kwa Wakuu
wa Kambi.

5. Kwa waombaji wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada zilizoainishwa
kwenye tangazo hili wanatakiwa kupakua (download) na kujaza fomu maalum
(Kiambatisho ‘B’) inayoonyesha taarifa zake binafsi.Bofya hapa
 
Fomu hiyo imeambatanishwa kwenye tangazo na inapatikana kwenye tovuti ya Polisi. Utumaji wa fomu hiyo uwe kwa njia ya ‘excel’ na usiwe kwa njia ya kuskani (pdf) isipokuwa barua za maombi na vyeti ndio viskaniwe (pdf). 
 
Kwa waombaji wa Tanzania Bara Maombi yatumwe kupitia barua pepe admin.phq@tpf.go.tz na kwa waombaji wa Zanzibar yatumwe kupitia barua pepe ajira.znz@tpf.go.tz. Maombi yatakayotumwa kwa mkono au kwa njia ya Posta
hayatopokelewa.

6. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/10/2023.
Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
S.L.P 961
DODOMA
09/10/2023

FANI ZINAZOTAKIWA KWA KILA NGAZI YA ELIMU SHAHADA
S/NO FANI
1 Architectures
2 Arts in French, Portuguese, Chinese and Arabs
3 Arts in Linguistics
4 Automobile Engineering
5 Boat Building
6 Civil Structural Engineering
7 Cyber forensic and Cyber security
8 Dental officer
9 Disaster Management
10 Electromechanics
11 Fibre glass
12 Laboratory science
13 Law Enforcement (BALE)
14 Marine Engineering
15 Marine Transportation
16 Master Fisherman
17 Mechatronic Engineering
18 Medical Doctor
19 Motor Vehicle Mechanics
20 Navigation
21 Physiology
22 Physiotherapy
23 Psychology
24 Quantity Surveyors
25 Radar Operation
26 Radar Technician
27 Radiology
28 Taxation
29 Theatre and Performing arts
30 Translation and Interpretation
31 Truck Mechanics

STASHAHADA
1 Architectures
2 Arts in French, Portuguese Chinese and Arabs
3 Aluminium Fitting and Fabrication
4 Automotive Air Condition
5 Electromechanics
6 Auto Electrical Engineering
7 Boat Building
8 Carpentry and Joinery
9 Cyber forensic and Cyber security
10 Electrical Engineering
11 Electrical installation and Industrial
12 Electronics and Telecommunication
13 Health Record management
14 Hotel management
15 Motor Cycle Mechanics
16 Motor Vehicle Mechanics
17 Navigation
18 Painting & Sign writing
19 Psychology
20 Radar Operation
21 Radar Technician
22 Refrigeration & Air Condition
23 Secretarial
24 Shipping and Logistic
25 Sound Engineering
26 Tailoring
27 Theatre and performing Arts
28 Truck Mechanics
29 Vehicle Programmer
ASTASHAHADA
1 Agriculture and Livestock
2 Aluminium fittings & Fabrications
3 Auto electrical Technician
4 Automotive Air Condition Technician
5 Boat Skippers
6 Body repair and Spray painting
7 Carpentry & Joinery
8 Car Interior Design Technician
9 Computer Application
10 Driving (class E & D)
11 Electrical Installation and Industrial
12 Electrical Technician
13 Electromechanics
14 Fitting and Turner
15 Hotel management
16 Information and communication Technology
17 Leather crafting
18 Mandatory course certificate
19 Masonry and Bricklaying
20 Mechanical Engineering
21 Mechatronic Engineering
22 Medical Records
23 Motor Cycle Mechanics
24 Motor Rewinding
25 Motor vehicle mechanics
26 Music and Sound production
27 Navigation
28 Nursing
29 Painting and Sign writing
30 Panel Beating
31 Performing Arts
32 Photocopy and Printer Maintenance
33 Plumbing and Pipe fitting
34 Quality manager
35 Records and Archive management
36 Refrigeration and Air Condition
37 Rescue Boat
38 Safety Manager
39 Scuba diving
40 Secretarial
41 Sewing Machine Maintenance
42 Sign Language
43 Sports (Football, athletics, Volleyball, Basketball, Handball, Boxing,
Judo, Karate and Swimming)
44 Tailoring
45 Truck Mechanics
46 Turning & fittings
47 Vehicle Programing
48 Welding & Fabrication

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news