IJP Wambura apangua makamanda wa polisi mikoa

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IJP Camillus Wambura anefanya uhamisho wa baadhi ya makamanda wa mikoa.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi makao makuu, SACP David Misime ambapo amefafanua kuwa, lengo la IJP Wambura ni kuboresha ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi.

Waliohamishwa ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Pili Mande aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ambaye anakwenda kuwa Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-Net) makao makuu Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ACP John Makuri ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.

Vile vile, Kamanda Msaidizi wa Polisi, ACP Debora Magiligimba aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala amehamishwa kwenda makao makuu ya Polisi Kitengo cha Polisi Wasaidizi.

Aidha, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Yustino Mgonja ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

Pia, IJP Wambura amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Mahamudu Banga aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Mara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news