Jenerali Mkunda aitaka SUMAJKT Bottling Company kuongeza ufanisi

DAR ES SALAAM-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ina matarajio makubwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Ni kutokana na jitihada mbalimbali ambazo imekuwa ikifanya ikiwemo ushirikiano, mipango na mikakati mizuri ambayo imekuwa ikisaidia kuongeza mapato na kuleta tija katika Taifa.

Jenerali Mkunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mikondo miwili ya uzalishaji na muonekano mpya wa chupa za maji ya Uhuru Peak sambamba na uzinduzi wa magari mawili kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa hiyo

Amesema, Serikali imekuwa na matarajio makubwa na Jeshi la Kujenga Taifa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akitembea kifua mbele kutokana na kuwa na chombo ambacho kinachotekeleza majukumu yake na kuiwezeaha nchi kuwa na amani.

"Matarajio yangu kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ni makubwa na weledi mliokuwa nao katika kutekeleza miradi mikubwa, imani yangu kwa jeshi ni kubwa natumaini amtaniagusha kama ilivyo kuwa ada na kuendelea kutimiza wajibu wanu kama ilivyo ada.

"Mnaweza kuona Serikali ilivyokuwa na imani na ninyi, nichukue fursa hii kuwapogeza na matarajio yangu ni makubwa kwenu,"alisisitiza Jenerali Mkunda

Jenerali Mkunda amesema,juhudi zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na jeshi kwa ujumla zimelenga kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za biashara na huduma katika Taifa kwa ujumla.

Amesema,Julai ulizinduliwa mradi wa Kituo cha Mafuta na leo hii anazindua mikondo miwili ya uzalishaji na bidhaa mpya ya maji ya kunywa na kueleza yote hayo yanatokana na jitihada, ushirikiano, mipango na mikakati mizuri ambayo imekuwa ikisaidia kuongeza mapato na kuleta tija ndani ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) pamoja Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa ujumla.

Aidha, alitoa wito kwa shirika kuendelea kubuni miradi mikubwa na kuboresha miradi na viwanda vilivyopo ili bidhaa zinazozalishwa ziweze kukidhi mahitaji ya ndani na nje ya nchi.

Pia aliwasii watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ufanisi ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

"Nitoe rai kwa watendaji kutunza miundombinu ya kiwanda hiki, ikiwa ni pamoja na kuzingatia ubora wa maji yanayozalishwa ili wateja wetu kote nchini waendelee kutumia na kufurahia maji haya ya kunywa ya Uhuru Peak na hivyo kuongeza mapato ya kiwanda,"alisema

Awali Mkurugenzi Mtendaji SUMAJKT, Kanali Petro Ngata amesema, mitambo hiyo yenye mikondo miwili imenunuliwa na kufungwa, ambapo mkondo wa kwanza una uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo 350 mls na 600 mls (kawaida na premier), lita 1 na lita 1.6. huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha chupa 10,000 kwa saa.

Amesema, kwa mkondo wa pili unazalisha maji makubwa yenye ujazo wa lita 13 na lita 18 pamoja na kuwa na uwezo wa kuzalisha chupa 500 kwa saa.

"Bidhaa hizi zimefanyiwa utafiti wa soko ili kukidhi matakwa ya wateja wetu Sambamba na ununuzi wa mtambo hii, Shirika lilifanya ukarabati wa majengo, kuboresha maabara, miundombinu ya umeme na ununuzi wa magari mawili (3.5 Tones) ambapo vyote kwa pamoja vimegharimu kiasi cha TShs 1,839,495,507.75,"amesema.


Aidha, amesema azma ya shirika ni kuhakikisha kampuni na miradi yake mbalimbali inakua na kuongeza vyanzo vya mapato vitakayowezesha shirika kutekeleza malengo yake kwa ufanisi zaidi.

Aidha, amesema uzinduzi wa bidhaa hizo mpya utaongeza wigo katika sekta ya Biashara na Huduma na kuongeza wateja, na kuliwezesja shirika kupata faida zaidi.

"Nitoe wito kwa Wakuu wa Kamandi, Vikosi, Shule, Vyuo pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutumia maji haya ya Uhuru Peak, kwani yana viwango vinavyokubalika Kitaifa na kimataifa,"amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Hassan Mabena akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Ofisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele amesema, kiwanda hicho cha maji ya kunywa cha SUMAJKT Bottling Company kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na uwezo mdogo kiuzalishaji.

Amesema, hali hiyo ilipelekea shirika kuweka mipango ya kuongeza Mikondo ya Uzalishaji ili kukidhi matakwa ya wateja wetu.

"Menejimenti ya shirika chini ya Bodi ya Ushauri ilipitisha mapendekezo ya maboresho na hatimaye kuagiza mitambo itakayowezesha kuzalisha bidhaa mpya za maji ambayo ikikupendeza utaizindua leo hii,"amesema.

Aliongeza kuwa,shirika linaendelea kutekeleza Mpango Mkakati wake wenye lengo la kuongeza mapato na faida kichumi na kijamii kwa kuboresha viwanda vilivyopo na kuanzisha viwanda vipya, ambavyo ni sehemu ya mipango ya shirika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news