Waziri Kairuki atoa wito kwa UNWTO kuzingatia usawa utoaji ajira

SAMARKAND-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb) ametoa wito kwa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) kuzingatia usawa katika kutoa ajira ikiwemo masuala ya kijinsia.

Wito huo umetolewa Oktoba 16, 2023 wakati akichangia mjadala katika Kikao cha Kamati ya Programu na Bajeti ya Shirika la Utalii Duniani, ambayo Tanzania ni mjumbe anayemaliza muda wake. Kikao hicho kimefanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani ulioanza leo jijini Samarkand, Uzbekistan.

Akichangia katika kikao hicho, Mhe. Kairuki ameelezea utayari wa Tanzania kuendelea kufanya kazi na Shirika la Utalii Duniani hususan kupitia miradi inayotekelezwa na Shirika hilo.

Aidha, Mhe. Waziri aliwashukuru UNWTO na UNDP kwa kuwezesha na kutoa mafunzo ya Kutangaza Utalii kwa njia za Kidigitali kwa Wadau wa Chama cha Wasafirishaji Watalii Tanzania (TATO). Vilevile, alipongeza juhudi za Mashirika hayo katika kuandaa Mkakati utakaounganisha Utalii na maendeleo ya kiuchumi kwa wazawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news