Mheshimiwa Mhagama atoa wito kwa UWT Songea

RUVUMA-Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini washauriwa kuendelea kuimarisha miradi ya uchumi ambayo itasaidia katika kuchechemua uhai wa miradi ya maendeleo ya Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya kata.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akicheza ngoma na wananchi katika Maadhimisho ya wiki ya (UWT) wilaya yaliyofanyika kata ya Maposeni Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, wakati wa Maadhimisho ya wiki ya (UWT) Wilaya ya Songea yaliyofanyika katika Kata ya Maposeni, jana tarehe 28/10/2023.

“Nimetoa kinu cha kupukuchulia Mahindi, kwa ajili ya (UWT) wilaya Songea; kama moja ya kitega uchumi kingine, naomba Kamati ya Uchumi kutumia miradi hii kuimaisha Ofisi ya (UWT) katika kata zote,”alieleza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akizungumza katika Maadhimisho ya (UWT) wilaya yaliyofanyika Kata ya Maposeni Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Aidha katika harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa (UWT) Wilaya ya Songea Vijijini, Waziri ametoa mabati ya ujenzi wa jengo zima na kiasi cha shilingi millioni moja kwa ajili ya gharama za ujenzi wa fundi.

Amefafanua kwamba lengo la kuanzishwa kwa (UWT) ni kumkomboa mwanamke; leo ni miaka 61 tangu tupate uhuru, leo wanawake tunasimama Mbele tumepata Rais Mwanamke na Mchapa Kazi.

“Mhe. Rais anajua mahitaji ya wanawake ya Msingi na mahitaji hayo pamoja na kuwasaidia wanawake yanawafaa pia na wanaume. Hakuna Rais amejenga vituo vingi vya Afya na zahanati nyingi kama Rais, Dkt. Samia Suluhu Hasssan,” amebainisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akikabidhi mabati katika wiki ya Maadhimisho ya (UWT) wilaya yaliyofanyika kata ya Maposeni Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Awali akizungumza wakati wa kukata keki ya Harambe, Mwenyekiti wa wa Kamati ya Uchumi ya Wilaya (UWT) Bi, Clementina Komba, ameomba wanawake kuamka na kupeana moyo katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa wanawake.

“Kamati ya uchumi tupo tayari kupita na kuelimishana kata kwa kata ili kujenga uelewa katika eneo ulilopo ni kitu gani ufanye ili kuimarisa uchumi,” alisema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ,(Mb) Peramiho akikabidhi daftari la usajili wa wanachama (UWT) wakati Maadhimisho ya kiwilaya yaliyofanyika kata ya Maposeni Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu; kufanya usafi wa mazingira kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari, kufungua daftari la (UWT) na usajili, na elimu ya kupinga ukatili na elimu ya uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news