Waziri Mavunde apokea changamoto za wachimbaji wadogo Itumbi

MBEYA-Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde apokea changamoto mbalimbali za wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Chunya mkoani Mbeya katika machimbo ya Itumbi akiwa katika ziara maalum ya kikazi.
Waziri Mavunde akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Mayeka Simon Mayeka alipokelewa na wachimbaji zaidi ya 200 ambao katika mkutano walitaja changamoto zao mbalimbali kama vile ukosefu wa mitaji, vifaa duni vya uchimbaji , ukosefu wa Nishati ya Umeme na kukosekana kwa Miundombinu salama.
Mapema baada ya kupokea changamoto hizo Mhe.Mavunde aliwatoa hofu wachimbaji kwa kuwaambia kuhusu mikakati mbalimbali iliyowekwa na Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo nchi nzima kwa kuwapatia mashine za uchorongaji, kuwaunganisha na taasisi za fedha ili kupata mikopo yenye riba nafuu na mpango wa kufanya utafiti wa kina ili kupata taarifa sahihi za miamba na madini.
Mhe.Mavunde amewataka wachimbaji wa Itumbi kujiunga na kujisajili rasmi katika vikundi ili watambulike na kuwekwa katika mikakati ya serikali itayowawezesha kujengewa wezo na kutatua changamoto zao.
Mhe .Mavunde amemuagiza Afisa Madini Mkazi Chunya ndugu Sabahi Nyansiri kusimamia na kuratibu zoezi hilo la kuunda vikundi na kuvisajili katika mifumo rasmi ili vitambulike na mamlaka husika.
Soko la Madini Wilayani Chunya lilianzishwa Mei 2, 2019. Kabla ya soko kuanza dhahabu iliyokuwa ikionekana katika takwimu za Serikali ni kilogramu 20 na baada ya soko kuanza wastani wa dhahabu inayopatikana kwa mwezi ni zaidi ya kilogramu 250.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news