Msigwa atoa wito Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa ametembelea Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichopo Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo.

Ziara hiyo imefanyika Oktoba 12, 2023 ambapo ameelekeza Watumishi wa Kituo hicho wafanye utafiti wa Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na kuandaa mkakati kabambe wa kutangaza kituo na majukumu yake kwa jamii.

Aidha, Katibu Mkuu amefurahishwa na namna kituo hicho kinavyohifadhi historia na kumbukumbu za Urithi wa Ukombozi ambazo ni Tunu ya Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news