Bodi ya Filamu nchini yatakiwa kushirikiana na sekta binafsi

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameilekeza Bodi ya Filamu nchini ishirikiane na sekta binafsi katika kuhakikisha filamu za Tanzania zinakua bora zaidi na zinapata soko la uhakika.
Dkt. Ndumbaro ametoa agizo hilo Oktoba 12, 2023 alipofanya ziara katika bodi hiyo, ambapo ameitaka iendelee kudhibiti na kufanya uhakiki wa ubora wa filamu ili kulinda mila na desturi za Tanzania.

Ameitaka bodi hiyo ibadilike na kwenda na wakati ili kupanua wigo wa kuwahudumia wadau wake kibiashara na kuongeza mapato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news