Msigwa awauma sikio wasanii kuhusu mikopo

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa ametoa rai kwa wasanii wawe mstari wa mbele kuulinda Mfuko wa Utamaduni na Sanaa kwa kufanya marejesho ya mikopo kwa wakati ili uweze kuendelea kuhudumia wengine.
Katibu Mkuu Msigwa ameyasema hayo Oktoba 13, 2023 alipotembelea Ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo alipata fursa ya kuzungumza nabaadhi ya wasanii ambao tayari wamenufaika na mikopo inayotolewa na mfuko huo.

"Hizi fedha zinategemea mzunguko kwa hiyo unapochukua mkopo hakikisha unarejesha kwa wakati ili wengine wapate na kuufanya hai wakati wote,"amesema Bw. Msigwa.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuinua sekta ya sanaa kwa kuwa ina umuhimu mkubwa sana kwa jamii hasa ikibadilishwa kuwa bidhaa inayoweza kurejesha utimamu wa mwili na akili kupitia burudani.

Amesema, sekta ya sanaa inaendana na mabadiliko ya teknolojia yanayowalazimu wasaniiwaeendelee kuhitaji huduma ya mikopo, hivyowana wajibu wa kuhakikisha wanaendelea kuthaminijuhudi za Serikali kwa kuutunza Mfuko huo.

Kwa upande wao Wasanii walionufaika akiwemo Muhsin Awadhi (Dkt.Cheni) na Abdul Msanga wakizungumza kwa nyakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuwathamani na kuanzisha mfuko huo ambao umewawezesha kupata mikopo kwa wakati na kufanya shughuli zao kwa ubora na thamani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news