Mwizi amchoma kisu tumboni, sikioni mwalimu wakati akimdhibiti mwenzake

RUVUMA-Mwalimu wa Shule ya msingi Njuga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, Emmanuel Ndunguru amenusurika kifo baada ya kuchomwa kisu tumboni na sikioni kutoka kwa mtu aliyekuja kumsaidia mwizi aliyemdhibiti.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Litola wilayani Namtumbo, Suleiman Runje amesema kuwa, mwalimu alivamiwa na mwizi nyumbani kwake.

Picha na Intaneti.

Na baada ya mwizi huyo kudhibitiwa na mwalimu mwizi mwingine aliingia na kumchoma kisu mwalimu Ndunguru na kumshinikiza mwalimu huyo kumwachia mwizi aliyemdhibiti.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Njuga, Yuster Kilowoko amedai mwalimu wake alipatwa na mkasa huo katika Kijiji cha Litola alikopanga na kuingiliwa na wezi waliopanga kuiba vifaa vilivyopo barazani kwake.

Kwa upande wake, mwalimu Emmanuel Ndunguru amesema alivamiwa na wezi usiku wa manane na baada ya kusikia kelele barazani kutokana na mwanguko wa vifaa vilimshtua na kuhisi kuwepo kwa wezi katika baraza yake na alipofungua mlango wake kuchungulia na kumwona kijana akihamisha vifaa hapo barazani alitoka kwenda kumkamata.

Mwalimu Ndunguru alifafanua kuwa, baada ya kumdhibiti mwizi huyo alipiga kelele kuomba msaada kwa majirani ili waje kuongeza nguvu kumdhibiti mwizi yule na badala yake aliingia mtu na kumchoma kisu yeye tumboni na sikioni akitaka amwachie yule mwizi aliyemdhibiti.

Kutokana na kitendo cha kuchomwa kisu tumboni kilimfanya mwalimu Ndunguru kutokwa na damu nyingi na kumwacha yule mwizi na wale wezi kuingilia kusikojulikana

Mwenyekiti wa Kijiji cha Litola, Suleiman Runje alidai mwalimu Emmanuel Ndunguru alichomwa kisu tumboni na sikioni na mtu aliyeingia ndani mwake baada ya mwalimu huyo kumkamata mwizi na baada ya kufikishwa Hospitali ya Peramiho alifanyiwa upasuaji na kushonwa sehemu aliyochomwa kisu.

Aidha, kwa sasa mwalimu huyo anaendelea vizuri na ameenda nyumbani kwake Mbinga kwa wazazi wake kwa ajili ya uangalizi wa karibu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news