Zanzibar mwenyeji Mkutano wa 20 wa Benki ya Dunia

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Nathan Balete na ujumbe wake Ikulu Zanzibar leo Oktoba 27,2023.
Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano uliopo kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uchumi wa buluu , sekta ya nishati hususani umeme wa jua, upepo na suala la gesi asilia, elimu, afya, kilimo, kujenga uwezo na msaada wa kiufundi, uwezeshaji wa wanawake, Mahakama na mengineyo.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Naye Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt.Saada Mkuya amesema, Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mkutano wa 20 wa mapitio wa Benki ya Dunia utakaoshirikisha wajumbe 350 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga kuanzia tarehe 06 hadi 08 Disemba mwaka huu katika Hoteli ya Golden Tulip Airpot Mkoa wa Mjini Magharibi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news