Naibu Waziri Kihenzile apigilia msumari stahiki za vibarua

DAR ES SALAAM-Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuhakikisha vibarua wanaofanya kazi katika Ujenzi wa Ofisi za Kanda ya Mashariki na Kituo cha Tahadhari za Tsunami wanapata stahiki zao kwa wakati ili kutokwamisha mradi huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mradi huo Naibu Waziri Kihenzile amesema kunyimwa haki kwa vibarua imekuwa ni moja ya sababu zinazowagombanisha wananchi na Serikali na kukwamisha miradi kukamilika kwa wakati.

“Miradi mingi inayotekelezwa nchini hususani kwenye Uchukuzi kumekuwa na malalamiko ya kutolipwa kwa vibarua na Makandarasi wanakuwa wameshalipwa sasa muhakikishe mnaisimamia kampuni inayojengwa ili pasiwe na malalamiko ya stahiki za vibarua hao,"amesema Naibu Waziri Kihenzile.

Naibu Waziri Kihenzile ameipongeza TMA kwa kuendelea kutoa taarifa za hali ya hewa kwa wakati hali inayosaidia wakulima na wajenzi kupanga mipango yao kwa kuzingatia taarifa hali ya hewa za wakati husika.

Aidha, Naibu Waziri Kihenzile ameitaka TMA kuongeza mbinu za utoaji wa elimu ili kuhakikisha kila mdau anafikiwa kwa wakati na kwa taarifa sahihi.

Kwa upande Wake Mshauri Mwelekezi Kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) John Malisa amemuhakikishia Naibu Waziri wa Uchukuzi Kihenzile kuwa hakuna sababu itakayochelewesha mradi kwani Mkandarasi amelipwa kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Burhan Nyenzi amesema TMA itaendelea kuboresha njia za mawasiliano ili kuwafikia wadau wote nchini ambapo kwa sasa wanafikiwa kupitia tovuti, taarifa kwa njia ya video, mitandao ya kijamii, mikutano na waandishi wa habari na ujumbe mfupi (SMS).

Mradi wa ujenzi wa Ujenzi wa Ofisi za Kanda ya Mashariki na Kituo cha Tahadhari za Tsunami unaojengwa na Kampuni ya Group Six Intendational ltd ya nchini China kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 30 na utagharimu takribani bilioni 9 na unatarajiwa kukamilika Julai mwakani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news