Waziri Prof.Mbarawa:TAA iwe na vyanzo vingi vya mapato


DAR ES SALAAM-Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) kuhakikisha TAA inakuwa na vyanzo vingi vya Mapato ili kutoa huduma nzuri zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati alipozindua rasmi bodi hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema uwepo wa vyanzo nje ya vile vinavyotozwa kupitia huduma za uendeshaji utaiwezesha TAA kuboresha viwanja vingi zaidi kwa muda mfupi.

“Kuna mapato mengi sana ambayo yanapatikana nje ya huduma za moja kwa moja zinazotolewa ndani ya Kiwanja, mkiweza kuja na mpango madhubuti kwenye eneo hilo TAA itafika mbali na itatimiza malengo yake kwa wakati,"amesema Waziri Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa ameitaka TAA kuhakikisha inapelekea watumishi wake kujifunza katika vya ndege mbalimbali duniani ili kuwaongezea ujuzi na utaalaam katika utendaji wa kazi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Juma Fimbo amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa watasimamia maeneo yote ikiwemo mifumo mipya iliyosimikwa viwanjani ili kutoa huduma za kisasa na viwango.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalawa na Rasilimali Watu Lucas Kambelenje maewapongeza wajumbe wa bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuwasisitiza kuzingatia miongozo.

Bodi ya TAA iiliyozinduliwa inajumuisha wajumbe inaongozwa na Mwenyekiti Juma Fimbo, Mhandisi Baraka Mwambage, Meshack Anyingisye, John Njawa, Plasduce Mbosa na Biseko Chiganga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news