Rais Dkt.Samia afanya mabadiliko ya uteuzi kwa Ma-DC, Ma-DED, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna TANAPA

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameteua na kufanya mabadiliko ya uteuzi kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala na Kaimu Kamishna (TANAPA) kama ifuatavyo:

1. Amemhamisha kituo cha kazi Mhe. Sixtus Raphael Mapunda kutoka Wilaya ya Sumbawanga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke. Mhe. Mapunda anachukua nafasi ya Bw. Mobhare Holmes Matinyi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

2. Amemhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Mhe. Kenan Laban Kihongosi kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba Mkoani Songwe.

Mhe. Kihongosi anachukua nafasi ya Bw. Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM.

3. Amemteua Bw. Elibariki Bajuta, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora badala ya Mhe. Kenan Laban Kihongosi ambaye amehamishiwa Momba.

4. Amemteua Bw. William Simon Mwakilema, Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Bw. Mwakilema anachukua nafasi ya Ndugu Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

5. Amemteua Ndugu Nyakia Ally Chirukile kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga ambapo anachukua nafasi ya Mhe. Sixtus Raphael Mapunda aliyehamishiwa Wilaya ya Temeke. Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nyakia alikuwa Katibu Tawala wa Ngorongoro.

6. Ametengua uteuzi wa Halfan H. Magani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe na badala yake kumteua Ndugu Goodluck Abinala Mwangomango. Kabla ya uteuzi huu Ndugu Mwangomango alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida.

7. Amemteua Bw. Said Majaliwa kuwa Mkurugenzi wa Tanga Mjini. Kabla ya uteuzi huu Ndugu Majaliwa alikuwa Mkurugenzi Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga.

8. Amemeteua Bw. Faraja Paschal Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kilindi Mkoani Tanga. Kabla ya uteuzi huu Bw. Msigwa alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

9. Amemteua Bi. Naima Bakari Chondo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Mjini. Bi. Naima anachukua nafasi ya Bw. Goodluck Abinala Mwangomango ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe.

10. Amemteua Bi. Shamim Adam Sadiq kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa. 11. Amemteua Bw. Hamza Hussein Hamza kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro ambapo anachukua nafasi ya Bw. Nyakia Ally Chirukile ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Hamza alikuwa Afisa Tarafa wa Ndudu, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. 12. Amemteua Bw. Lameck Karanga Ng’ang’a kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Bw. Ng’ang’a ambaye alikuwa Katibu Tarafa Karatu anachukua nafasi ya Msigwa aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilindi.

13. Amemteua Bw. Musa N. Kuji kuwa Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA). Bw. Kuji alikuwa Naibu Kamishna wa Huduma za Shirika (TANAPA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 3, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news