Rais Dkt.Samia afanya uteuzi Tume ya Kurekebisha Sheria, BASATA na MoCU

DOHA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Bw. George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mandepo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Bw. Mandepo anachukua nafasi ya Mhe. Griffin Venance Mwakapeje ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

ii) Amemteua Dkt. Saudin Jacob Mwakaje kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Dkt. Mwakaje ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza lililomaliza muda wake.

iii) Amemteua Bw. George Daniel Yambesi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kipindi cha pili. Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Oktoba, 2023.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 2,2023 jijini Doha nchini Qatar na Mkurugenzi wa Mawasiano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news