Sasa ni zamu ya vijiji vya Nyambono, Kaburabura ujenzi wa zahanati

NA FRESHA KINASA

WADAU mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wazawa wa Kijiji cha Nyambono Kata ya Nyambono na Kijiji cha Kaburabura Kata ya Bugoji katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara wameombwa kujitokeza kuchangia ujenzi wa zahanati mpya zinazojengwa katika vijiji vyao.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Oktoba 5, 2023 ambapo hatua hiyo itasaidia wananchi hao waweze kupata huduma za afya karibu na makazi yao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika kuhakikisha zanahati hizo mpya zinajengwa katika vijiji hivyo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof.Sospeter Muhongo ataambatana na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) ya Musoma Vijijini kuchangia na kuhamasisha ujenzi wa zahanati mpya za vijiji hivyo.

Kwa mujibu taarifa hiyo Alhamisi ya Oktoba 12, 2023 majira ya saa 4 asubuhi itakuwa katika Kijiji cha Nyambono kilichopo Kata Nyambono na siku hiyo hiyo majira ya saa 9 alasiri itakuwa katika Kijiji cha Kaburabura Kata ya Bugoji.

"Wadau wetu wa maendeleo wakiwemo wazaliwa wa vijiji/kata hizo wanaombwa kuchangia miradi hiyo ya ujenzi wa zahanati za vijiji hivyo. Karibuni Sana kwenye harambee za maendeleo ya Vijijini mwetu." imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news