Serengeti yashinda Tuzo ya Hifadhi Bora Afrika kwa mara ya tano mfululizo

DUBAI-Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Tuzo ya Hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2023(Africa’s Leading National Park 2023).

Hii inakuwa ni mara ya tano mfululizo kushinda tuzo hiyo baada ya kuwagaragaza washindani wa tuzo hii kama Central Kalahari Game Reserve- Botwswana, Etosha National Park -Namibia, Kidepo Valley National Park -Uganda, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve - Kenya.

Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ usiku wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika Hoteli ya Atlantis The Royal Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu na kupokelewa na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai, kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news