Tanzania na Uzbekistan kushirikiana Sekta ya Utalii

SAMARKAND-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana wa jimbo la Kharezm jijini Samarkand nchini Uzbekistan, Bw. Davletov Anvar Kenjayevich.

Majadiliano hayo ambayo yameangazia kuhusu ushirikiano katika sekta ya utalii baina ya Tanzania na Uzbekistan yamefanyika Oktoba 15, 2023.
Waziri Kairuki pia atapata nafasi ya kutembelea Chuo Kikuu cha Utalii ili kuona uzoefu wa Uzbekistan katika mafunzo ya sekta ya utalii; na kutafuta nafasi za kujengewa uwezo kutoka kwao hasa ikizingatiwa kuwa jiji la Samarkand limeendelea kiutalii.

Vilevile, Mhe. Kairuki na ujumbe wake wanatarajia kuona uzoefu ilionao Uzbekistan katika uratibu wa makumbusho za Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news