TARURA yaunganisha wananchi wa Liwale na Nachingwea

LINDI-Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Lindi inaendelea na kazi ya kuunganisha na kufungua barabara katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Liwale, Mhandisi Livingstone Shija amesema kuwa malengo ya TARURA katika Wilaya hiyo ni kuhakikisha wananchi wanasafiri kwa urahisi ili kuzifikia huduma za kijamii na kiuchumi.

Katika kuhakikisha hilo, TARURA imefanya matengenezo ya Barabara ya Liwale-Lilombe - Mbwemkuru yenye urefu wa Kilomita 83 ambapo kati ya hizo kilomita 20 zimefunguliwa.
"Mwanzoni wananchi wa Lilombe walipotaka kwenda Nachingwea walitakiwa kuanza kufika Liwale mjini ndipo wapate magari ya kufika Nachingwea lakini kwa sasa wanatoka Lilombe na kufika Nachingwea moja kwa moja na magari yapo,"amesema Mhandisi Shija.
Naye Bw. Emmanuel Kimswale mkazi wa Kijiji cha Majonanga ameipongeza serikali kwa matengenezo ya barabara hiyo ambayo inarahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news