WATANZANIA WAASWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MAONESHO YA DAR CONSTRUCTION EXPO ILI KUJIFUNZA TEKNOLOJIA MPYA ITAKAYOPATIKANA KATIKA SEKTA YA UJENZI

DAR ES SALAAM-Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi na Muandaaji wa Maonesho hayo, Bw. Deogratius John Kilawe , alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa,maonesho hayo yana lengo la kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa Sekta ya Ujenzi na kujadili njia mbalimbali zitakazosaidia kuinua sekta hiyo pamoja na kukuza mahusiano na kujipatia wateja wa bidhaa zao.
Pia amesema, maonesho haya yanatarajiwa kuwa ni ya siku tatu kuanzia tarehe 11- 13 Oktoba 2023 na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Aidha,Bw. Kilawe amesema kuwa, huu ni msimu wa 7 wa Maonesho ya Dar Constuctions Expo na yanajumuisha zaidi ya Makampuni 120 kutoka nje na ndani ya Tanzania pia yanatarajiwa kuwa yenye kuleta tija na mapinduzi katika sekta ya ujenzi na kukuza;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news