Waziri ashiriki Mkutano wa Mwaka wa Merck Foundation nchini India

MUMBAI-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ni kati ya viongozi wanaohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Merck Foundation inayoshughulika na masuala ya kijamii, afya na kiuchumi unaofanyika Oktoba 18-19, 2023 jijini Mumbai India.

Lengo la Mkutano huo ni kujadili mikakati na programu kuhusu huduma za kijamii kwa Wanawake zikiwemo afya na elimu kwa watoto wa kike husuan ni kutokomeza unyanyapaa kwa wenye tatizo la ugumba barani Afrika na nchi zinazoendelea.

Kutoka nchini Tanzania, Waziri Dkt. Gwajima atawasilisha taarifa ya Tanzania kuhusu ushirikiano na Merck Foundation na baadaye atashiriki katika majadiliano yanayolenga kuwainua wanawake kiuchumi, kijamii na kuainisha mikakati inayofanywa na nchi kuhusu kundi makundi maalum wakiwemo wagumba.

Taasisi hiyo inawakutanisha watoa huduma za afya, watunga sera, wasomi, watafiti na vyombo vya Habari vya afya zaidi huku ukifuatiliwa na zaidi ya watu 6000 kutoka nchi 70 zikiwemo Afrika, Asia na nchi nyingine duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news