Waziri Kairuki aongoza Mkutano Mkuu wa 23 wa UNWTO nchini Uzbekistani

SAMARKAND-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, (Mb), leo tarehe 18 Oktoba, 2023 ameongoza Mkutano Mkuu wa 25 wa UNWTO unaoendelea Jijini Samarkand, Uzbekistani. 
Hatua hiyo imefuatia kuthibitishwa kwaTanzania na Nchi Wanachama kuwa Makamu wa Rais wa Mkutano huo.

Akiongoza Mkutano Mkuu wa UNWTO Mhe. Kairuki amezishukuru nchi wanachama wa UNWTO kwa kuichagua nchi ya Tanzania katika nafasi ya Makamu wa Rais na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na nchi hizo ili kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii duniani.

Mkutano huo unaoendelea nchini Uzbekistani ulifungulia tarehe 16 Oktoba, 2023 na Rais wa Uzbekistan, Mheshimiwa Shavkat Mirziyoyev na unahudhuriwa na Mawaziri wa Utalii kutoka Nchi wanachama wa UNWTO zaidi ya 121 pamoja na Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za kifedha na wadau kutoka sekta binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news