Waziri Dkt.Ndumbaro ateta na Mwenyekiti wa Bodi ya BASATA

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Prof. Saudin Mwakaje jijini Dar es Salaaam.
Mhe. Ndumbaro amempongeza Prof Mwakaje kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza Baraza hilo, akimtaka ahakikishe baraza linaendelea kuwa mshauri na mlezi katika Sekta ya Sanaa na kutekeleza majukumu yake mengine kwa manufaa ya wadau wa Sekta hiyo.

Kwa upande wake Prof.Mwakaje amemshukuru RaisDkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasialiyompatia ya kuongoza Baraza hilo kwa nafasi ya Mwenyekiti na kuahidi kusimamia Baraza hilo kutekeleza majukumu yake ipasavyo, kwa kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao pamoja na kuongeza mapato kwa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news