Mikutano ya Kimataifa ni fursa ya kukitangaza Kiswahili-Dkt.Ndumbaro

ARUSHA-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema, mikutano ya Kimataifa inayofanyika hapa nchini ni fursa ya kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili ambayo ni mojawapo ya Lugha Rasmi ya Kikazi ya Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Jumuiya kadhaa za Kikanda barani Afrika.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 7, 2023 jijini Arusha katika kikao cha Maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9, 2023 jijini Arusha.

Mhe. Ndumbaro ameongeza kuwa, Tanzania ina wataalamu katika tafsiri na ukalimani, hivyo wana uwezo wa kutoa huduma ya ukalimani katika mikutano hiyo.

Kikao hicho kimeongozwa na Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana,Waziri wa Katiba na Sheria na kuhudhuriwa na Mhe.Haroun Suleimani,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news