Zanzibar itafunguka kwa barabara za lami, fly over-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, anatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa ujenzi wa barabara za aina barabara za mijini, vijijini na za kuunganisha mikoa na wilaya zake.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Oktoba 25,2023 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kuelekea shamrashamra za miaka mitatu ya uongozi wake alipoweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa barabara ya Jozani, Ukongoroni- hadi Bwejuu za kilomita 23.3 Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, kuna mradi mkubwa wa barabara zote za Mjini Unguja dola za Marekani milioni 100 zenye kilometa 100.9 yakiwemo madaraja mawili ya juu, Mwanakwerekwe na Amani kwa barabara za kisasa.

Vilevile Mkoa wa Kusini Unguja ujenzi wa barabara za njia nne kutoka Tunguu mpaka Makunduchi kwa barabara mpya na kisasa zenye taa .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news