Zingatieni umuhimu wa afya ya akili ili kuzuia maafa-Waziri Riziki Pembe

ZANZIBAR-Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kuzingatia umuhimu wa afya ya akili ili kuzuia maafa ambayo yanayoweza kutokea na kupelekea athari kubwa kwa katika mwili wa binadamu.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma akizungumza katika bonanza la kuadhimisha kuelekea siku ya afya ya akili na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha Afya Zanzibar Wilaya ya Magharib “B” Unguja, Oktoba 9,2023.

Akizungumza katika bonanza la kuadhimisha kuelekea siku ya afya ya akili na maafa duniani lilofanyika katika jengo la Chuo cha Afya Zanzibar Wilaya ya Magharib “B” Unguja amesema, kila mwananchi anapaswa kutambua umuhimu wa afya ya akili kama ilivyo afya ya mwili ili kujikinga na maafaa ambayo yanawezakujitokeza.

Amesema, afya ya akili ni muhimu kwa kila mtu kwani inamuwezesha kuishi maisha yenye furaha, tija na kujisikia vizuri ulimwenguni.

Lakini mara nyingi suala hili halipewi kipaumbele kinachostahili. Hivyo Waziri huyo amehimiza suala la afya ya akili kupewa kipaumbele na kila mtu, kutambua kwamba ni sehemu muhimu ya afya kwa ujumla.
“Afya ya Akili ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kwani maafa hayachagui mtu wa kumuathiri, yanaweza kumuathiri mtu yeyote, mahali popote, wakati wowote,"amesema Waziri Pembe.

Alifahamisha kwamba kila ifikapo tarehe 10 Oktoba, huadhimishwa Siku ya Afya ya akili na maafa Duniani, siku hii inawakumbusha watu/jamii juu ya umuhimu wa kuwa tayari katika kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea. Pia alisema siku hiyo huongeza uelewa wa afya ya akili na kuleta mabadiliko chanya kwa afya ya akili ya kila mtu.

Aidha, Waziri Pembe alisema mwaka huu 2023, katika kuadhimisha Kimataifa siku ya Afya ya akili itachunguza uhusiano wa pande mbili kati ya maafa na usawa wa kijinsia, hivyo amewaomba wananchi kupenda kukuhimizana kushiriki katika kila tukio la kuendeleza umoja, au kujiunga na mazungumzo juu ya kupambana na usawa wa kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji Chuo cha Afya Zanzibar (ZSH), Aziza Hemed ametoa wito kwa wananchi kuwa mabalozi wazuri kuhamisha jamii kupata ushauri nasihi na kisaikolojia pale ambapo wanapopata matatizo za kimaisha kwani hatua hiyo inaweza kupunguza athari za maafa ambazo zinatokana na binadamu.

Kupitia bonanza hilo shughuli mbali mbali zimeandaliwa ikiwemo debeti,michezo,utowaji wa zawadi pamoja na zoezi la kuhitimisha program ya mafunzo ya msingi “Crash Program”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news