Waziri Mhagama awapa kongole Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu

MANYARA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama afurahishwa na ushiriki wa ofisi yake katika uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani yanaendelea katika Viwanja vya Standi ya Zamani Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza alipotembelea banda la Ofisi yake wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani. Maonesho hayo yanaendelea katika Viwanja vya Standi ya Zamani Babati mkoani Manyara.

Maonesho hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambapo yameambatana na uwepo wa maonesho mbalimbnali, shughuli za uzalishaji katika kuipamba wiki ya vijana inayozinduliwa tarehe 10 Oktoba, 2023 Wilayani humo Mkoani Manyara.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhandisi Cyprian John Luhemeja alizungumza jambo mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani. Maonesho hayo yanaendelea katika Viwanja vya Standi ya Zamani Babati Mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mratibu wa masuala ya UKIMWI Kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) Bw. Gilbert Mbwambo alipotembelea banda hilo kujionea shughuli za Tume hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama Pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa kwanza kulia) wakitembelea mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani. Maonesho hayo yanaendelea katika Viwanja vya Standi ya Zamani Babati Mkoani Manyara.
Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Numpe Mwambenja akitoa maelezo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa kwa wananchi waliotembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana pamoja na maadhimisho ya kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa Duniani. Mratibu wa Maafa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Khowe Malegeri akitoa elimu kuhusu hatua za kuchukua kukabiliana na uwepo wa mvua za El nino zilizotabiriwa kwa wananchi waliotembelea banda la Ofisi hiyo katika maonesho yanayoendelea Babati Manyara.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Waziri Mhagama amepongeza maandalizi yaliyofanywa na kuendelea kuisihi ofisi hiyo kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu uwepo wa mvua za El nino nchini kwa kuzingatia utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news