Abiria 25 wajeruhiwa, 13 wafariki ajali iliyohusisha basi kugonga kichwa cha treni Singida

DAR ES SALAAM-Ajali ya basi mali ya Kampuni ya Ally's Star na treni iliyotokea alfajiri leo Novemba 29, 2023 mkoani Singida imeua watu 13 na kujeruhi wengine 25.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), imesema ajali hiyo imehusisha basi la abiria lenye namba T178 DVB mali ya kampuni hiyo kugonga kichwa cha treni chenye namba V951 9006 kilichokuwa kikitokea Stesheni ya Aghondi kuelekea Manyoni katika makutano ya reli na barabara eneo la Manyoni mkoani Singida.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk ameeleza kuwa,“Ajali imehusisha basi la abiria lililokuwa likivuka njia ya reli eneo la kilomita 587 Manyoni na kichwa cha treni na kusababisha majeruhi 25, wanawake 7, wanaume 18 na vifo vya watu 13, wanawake 6, wanaume 7.

"Shirika linatoa pole kwa ndugu wa marehemu na Mwenyezi Mungu awape nafuu majeruhi waweze kuendelea na shughuli za kujenga taifa.”

Taarifa hiyo imesema TRC itaendelea kuutaarifu umma kadiri taarifa zinavyopatikana na kushauri madereva kuheshimu sheria za barabarani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news