Balozi Mbarouk ampongeza Spika Dkt.Tulia kwa ushindi urais IPU

DODOMA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Balozi Mbarouk aliambatana na Mabalozi watatu waliohusika kwenye Kampeni ya IPU walipoenda kumpongeza kwa ushindi huo na kumhakikishia Ushirikiano wa Wizara katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.
 
Mabalozi watatu ni pamoja na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Seiman Suleiman, Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva, Balozi Hoyce Temu pamoja na Balozi Robert Kahendaguza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news