Dkt.Kikwete amwakilisha Rais Dkt.Samia katika maziko ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa Finland

HELSINKI-Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya maziko ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. 


Wakati wa kutoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa, Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Mhe. Sauli Niinistö,familia ya marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mashuhuri duniani.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akimpa pole Mjane wa Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari.

Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Mhe. Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Finland, Mhe. Sauli Niinistö wakati wa hafla alyoiandaa kwa viongozi na wageni walioshiriki Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa nchi hyo, Hayati Martti Ahtisaari yaliyofanyika tarehe 10 Novemba 2023.

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na viongozi na waombolezaji wengine katika hafla ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. Rais Kikwete alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.

Katika vipindi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news