Dkt.Mollel:Tuendelee kumuombea Rais Dkt.Samia

KILIMANJARO-Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa waumini wa Msikiti wa Sanya Juu Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza taifa kwa amani na utulivu.

Dkt. Mollel ametoa wito huo katika maadhimisho ya Siku ya Elimu ya Dini katika Msikiti wa Sanya Juu wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.

Dkt. Mollel amesema Taifa lenye amani na utulivu wananchi wake wanafanya kazi kujipatia kipato ili kuleta maendeleo ya taifa lao.

“Rais Samia ni kiongozi imara na shupavu hivyo watanzania ni kumtia moyo kwa kumuombea ili awezetimiza yale alopanga kuyatekeleza katika kuleta maendeleo kwa watanzania na Tanzania isonge mbele,”ameeleza Dkt.Mollel.

Aidha, Dkt.Mollel ameupongeza uongozi wa msikiti huo kwa kuwalea watoto katika maadili mema na kusema kuwa hao ndo viongozi wa kesho watakao kuja kulitumikia taifa.

Vile vile amewatia moyo walimu wanao fundisha watoto katika msikiti huo kwa kuwapatia kiasi cha shilingi million moja ili kuendelea kuwafundisha watoto hao kwani ndio taifa la kesho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news