Kisiwa cha Rukuba waamua kujenga shule, Prof.Muhongo awaunga mkono

NA FRESHA KINASA

WAKAZI wa Kisiwa cha Rukuba kilichopo Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara wameamua kujenga sekondari yao ili elimu ya sekondari itolewe hapo kisiwani badala ya wanafunzi kwenda kupanga vyumba nchi kavu huko Kijiji cha Etaro kwa ajili ya elimu ya sekondari.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 1, 2023 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijni chini ya Prof. Sospeter Muhongo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,sekondari mpya tano zinajengwa kwenye vijiji vitano katika Kisiwa cha Rukuba (Kata ya Etaro), Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), Kurwaki (Kata ya Mugango), Muhoji (Kata ya Bugwema), na Wanyere (Kata ya Suguti) ambapo serikali inagharamia ujenzi.

"Harambee ya kwanza ya ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba ilishafanyika chini ya usimamizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, akishirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini,"imeeleza taarifa hiyo na kuongeza,

"Ujenzi umeanza matofali 2,900 tayari yametengenezwa na kila mfuko mmoja wa saruji umetoa matofali 25. Huku ujenzi wa vyumba viwili na ofisi moja ya walimu umeanza msingi wa mawe unajengwa.

"Tafadhali sana tunaomba mchango wako. Akaunti ya kuweka mchango wako wa fedha ni: Benki ya NMB namba: 30302300701 Jina la Akaunti: Serikali ya Kijiji cha Rukuba.

"Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wamedhamiria kujenga sekondari kisiwani humo ili kuboresha upatinakaji wa elimu ya sekondari kwa watoto wao,tuwaunge mkono."

Prof.Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ameishachangia saruji mifuko 100 na pia ametoa tena saruji mifuko 50 na ataendelea kuchangia ujenzi huo.

Jimbo la Musoma Vijijini lina kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374. Jimbo hili lina jumla ya sekondari 25 za kata ambazo zinamilikiwa na Serikali, mbili za binafsi chini ya Katoliki na SDA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news