Maji safi na salama yazidi kusambazwa Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

ZOEZI la usambazaji wa maji ya bomba katika Jimbo la Musoma Vijiji Mkoa wa Mara kwa lengo la kuhakikisha wananchi jimbo humo wanapata maji safi na salama linazidi kushika kasi kila kona jimboni humo.

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini pamoja na Mheshimiwa Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo wamesema kuwa, wanamshukuru Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake na dhamira yake njema ya kutoa fedha za usambazaji wa maji safi na salama.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Novemba 19, 2023 imebainisha kazi za mwezi Septemba hadi Novemba, mwaka huu wa 2023.

1. Kazi za BADEA:

-Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

-Mradi wa Tsh 70.5 bilioni,

Lita 17.5 milioni za maji zitazalishwa kweye Chujio. Maji ya bomba hili yatasambazwa Musoma Vijijini (Kata za Mugango, Tegeruka, Busambara, Kiriba na Ifulifu). Na Vifaa vya kukamilisha mradi kutoka Uturuki na China vimeanza kuwasili nchini

2. KAZI ZA MUWASA

2i. Kata ya Tegeruka: Vijiji vya Tegeruka, Mayani na Kataryo vimetandaziwa mabomba. Kazi hii ya utandazaji mabomba ni endelevu, yaani inaendelea.

2ii. Kijiji cha Mkiriri kimefikishiwa maji ya bomba

2iii. Vijiji vya Nyegina na Kurukerege vinakamilishiwa miundombinu ya kupata maji ya bomba.

MUWASA inasambaza maji ya bomba kwenye Kata 4 (Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu) za Musoma Vijijini kutoka kwenye chanzo chake cha maji kilichoko Bukanga, Musoma Mjini.

3. KAZI ZA RUWASA

3i. Maji ya Chumwi- Mabuimerafuru

Tenki lenye ujazo wa Lita 300,000 limejengwa Kijijini Mabuimerafuru. Maji ya Tenki hili yatasambazwa kwenda: (a) Vijijini Mabuimerafuru na Chumwi, na (b) Vijijini Masinono na Bugwema

3ii. Maji ya Kata ya Bwasi

Tenki la ujazo wa Lita 150,000 limejengwa Kijijini Bwasi. Maji ya Tenki hili yatasambazwa Vijijini Bwasi, Kome na Bugunda. Chanzo cha maji ya Kata ya Bwasi ni maji ya bomba la Bujaga/Bulinga

3iii. Miradi ya Kata za Busambara na Kiriba: matangazo ya kumtafuta Mkandarasi yametolewa

KUKUMBUSHA

Vijiji vyetu vyote 68 vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria, na utekelezaji wake uko kwenye hatua mbalimbali. Taarifa za utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa maji ya bomba vijijini mwetu zitaendelea kutolewa.

SHUKRANI

"Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Mhesgimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za usambazaji wa maji safi na salama vijijini kwetu,asante sana,"imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news