Mataifa ya Kiarabu kukutana kwa dharura Novemba 11, 2023

RIYADH-Kikao cha dharura cha Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Viongozi wa Mataifa ya Kiarabu kitafanyika Jumamosi ya Novemba 11, 2023 chini ya urais wa Saudi Arabia huko jijini Riyadh.

Muonekanao wa Riyadh ambao ni mji mkuu na mji mkubwa zaidi wa Saudi Arabia. Jina Riyadh linatokana na wingi wa neno la Kiarabu rawdha, ambalo linamaanisha bustani.(Picha na Shutterstock).

Sekretarieti Kuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetangaza kwamba, imepokea ombi rasmi kutoka Palestina na Saudi Arabia la kufanya kikao kisicho cha kawaida cha Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika ngazi ya mkutano huo, Al-Sharq Bloomberg iliripoti Jumanne. Saudi Arabia inaongoza kikao cha sasa cha 32 cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

Balozi Hossam Zaki, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema kuwa, Sekretarieti Kuu ilipokea siku ya Jumatatu ombi rasmi kutoka Palestina na Saudi Arabia la kufanya mkutano huo.
 
Lengo likiwa ni kujadili uchokozi unaoendelea wa Israel dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza. Amesema kuwa, Sekretarieti Kuu imesambaza taarifa kuhusu mkutano huo kwa nchi wanachama wa Kiarabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news