Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZSHF) watoa darasa kwa wanachama

NA FAUZIA MUSSA
MAELEZO

WANACHAMA wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZSHF) wametakiwa kufuata sheria na miongozo ya ZHSF ili kuzifanya huduma hizo kuwa endelevu.

Mkurugenzi Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), Asha Kassim biwi akizungumza na watendaji wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya mfuko huo huko Maruhubi Mjini Unguja.

Akizungumza na watendaji wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya Mfuko huo Afisa Masoko na Uhusiano, Asha Kassim Biwi alisema, mfuko huo umeanzishwa chini ya Sheria Na.1 ya mwaka 2023 kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu, pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha kwaajili ya kugharamia huduma hizo.
Aidha, alisema kwa mujibu wa Sheria hiyo mfuko una Jukumu la kukusanya ,kuhifadhi na kusimamia fedha hizo ili kulipia gharama za matibabu kwa Wanachama na Wategemezi wao.

Alifahamisha kuwa Mfuko huo haukuwalenga watendaji wa Serikali tu kwani sheria ya mfuko imewagawa wanachama kwa makundi kulingana na kipato cha mwanachama husika.

Akizungumzia kuhusu makosa na adhabu katika sheria hiyo amesema sheria inaelekeza kutolewa adhabu kwa mwanachama atakaekwenda kinyume na sheria za mfuko au kufanya uhujumu ikiwemo faini, kifungo au vyote kwa pamoja,hivyo aliwataka Wanchama hao kutumia kadi zao pale tu inapohotajika ili kuepusha usumbufu usio wa lazima.

Ofisa Idara ya uvuvi Ali Khamis Shadhil akiuliza maswali kwa maofisa wa mfuko wa huduma za Afya wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya sheria ya mfuko huo.

Amesema, kila mmoja ana jukumu la kuulinda mfuko huo, pamoja na kuchangia afya ili kuimarisha na kurahisisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu nchini.

“Utakapoimarisha Afya ya Taifa umeimarisha Uchumi, bila ya Afya hakuna maendeleo hakuna wafanyakazi, wavuvi, wakulima kwa hali hii uchumi utadumaa,”alifahamisha Mkuu huyo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru ZHSF kwa kuwafikia na kuwapatia elimu inayoenda kuharakisha utendajikazi wa mfuko huo.

Walisema tayari ZHSF imeshatoa orodha ya Hospitali zinazotoa huduma hizo na taratibu zake hivyo wapo tayari kufuata utaratibu huo ili kuepusha changamoto zisizo za lazima.

Sheria ya mfuko wa huduma za Afya ZHSF ilipitishwa Barazani febuari 28 2023 na kutiwa saini na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi Machi 20,2023 na kuchapishwa rasmi katika gazeti la Serikali Machi 30 mwaka huohuo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news