ZURA yatangaza bei ya mafuta Zanzibar kwa Novemba 2023

ZANZIBAR-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei za mafuta kwa mwezi Novemba 2023 ambazo zimeanza kutumika rasmi Novemba 9, 2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano ZURA, mamlaka hiyo hupanga bei kwa kuzingatia mambo mbalimbali.

Mosi, ni wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei ya mafuta duniani, pili gharama za uingizaji mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam na Tanga.

Tatu, thamani ya shilingi ya Tanzania kwa dola ya Marekani, nne gharama za usafiri, bima na premium hadi Zanzibar.

Tano, kodi na tozo za Serikali na sita ni kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja kote Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news