Mungu awabariki sana NHC, mmekuwa kimbilio letu-Halilli

DAR ES SALAAM-Taasisi ya Haki sawa kwa Watu wenye Ulemavu (Equal Rights for People with Diabilities) yenye makao makao yake makuu Mtaa wa Kanuni, Mabibo, Dar es Salaam, imelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa msaada wa vitu mbalimbali ilivyotoa kwa taasisi hiyo.

"Mungu, awabariki sana NHC, hii siyo mara kwanza kufanya hivi, mmekuwa kimbilio letu na huwa hamtuachi, mmekuja wakati muafaka sana ikizingatiwa kuwa hiki ni kipindi cha mvua ambacho kina changamoto sana hususani kwenye suala la mwendo Kwa watu wenye ulemavu,"alisema Said Mrisho Halilli ambaye ni Makamu Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Equal Rights for People with Diabilities.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo,Said Mrisho Halilli, akizungumza muda mchache baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo na timu kutoka NHC, makao makuu ya Chama hicho.

Katika hatua nyingine, Taasisi hiyo imetoa wito kwa Mashirika ya Umma kama NHC na ya Sekta binafsi, kuiga mfano wa NHC kwa kutoa msaada huo bila kusubiri msimu wa sikukuu ama maadhimisho husika, kwakuwa mahitaji yao ni ya wakati wote.

Kwa upande wa NHC, Yahya Charahani, ambaye ni Afisa Uhusiano Mkuu kutoka Kitengo cha Uhusiano na Habari cha shirika hilo akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, amesema, ni utaratibu wa NHC, wa kurejesha kidogo inachopata kwa jamii lakini kubwa ni utekelezaji wa kisheria wa suala hili kwa lugha ya kimombo Corporate Social Responsibility (CSR).





Msaada huo wa NHC, umejumuisha fimbo kwa watu wenye ulemavu wa macho, vifaa saidizi kwa ajili ya viwiko, mafuta ya kukinga ngozi dhidi ya miale mikali ya jua na vifaa saidizi kwa ajili ya mwendo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news