Rais Dkt.Mwinyi afanya mahojiano na Benny Mwaipaja kuelekea IDA20 Mid-Term Review


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, baada ya kufanya mahojiano maalumu kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wa Kati wa Mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid-Term Review) utakaofanyika Zanzibar, kuanzia tarehe 6 hadi 8 Desemba, 2023, ukiwashirikisha wajumbe zaidi ya 300 kutoka mataifa takribani 100 duniani. 
 
Katika mahojiano hayo, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi, amewakaribisha washiriki wa mkutano huo nchini Tanzania hususan, katika Visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar), ili kushuhudia Maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii yaliyofikiwa kupitia mikopo nafuu na misaada kupitia Benki ya Dunia na amewataka wananchi kuchangamkia fursa za ugeni huo katika Sekta mbalimbali ikiwemo utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news